#HABARI:Wananchi wa Chanika, katika wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, wamesema kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia i…

#HABARI:Wananchi wa Chanika, katika wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, wamesema kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia i…

#HABARI:Wananchi wa Chanika, katika wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, wamesema kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia imeleta matumaini makubwa ya kupatikana kwa muafaka katika mgogoro wao wa muda mrefu, na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kuhusu eneo la msitu wa Kazimzumbwi.

Wakizungumza na ITV, wananchi hao wamesema mgogoro huo, ambao umedumu kwa takribani miaka 25, umekuwa ukihusisha madai ya wananchi hao kuvamia eneo la msitu huo, wa hifadhi huku zaidi ya wananchi 10,000 wakiwa ni wahanga.

Naye Mratibu wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, Dkt. Baraka Mkami, amesema kuwa kampeni hiyo imeweza kuwafikia wananchi takribani 400, kwa kuwapatia elimu ya kisheria, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mivutano na kuanzisha mazungumzo ya kutafuta suluhu ya kudumu.

#Follow RadioOneStereo

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *