#HABARI: Zaidi ya wanawake 100 wafanyabiashara wa chakula wa kata zote 4 za Tarafa ya Pawaga wamepata mitungi ya gesi kupitia ka…

#HABARI: Zaidi ya wanawake 100 wafanyabiashara wa chakula wa kata zote 4 za Tarafa ya Pawaga wamepata mitungi ya gesi kupitia ka…

#HABARI: Zaidi ya wanawake 100 wafanyabiashara wa chakula wa kata zote 4 za Tarafa ya Pawaga wamepata mitungi ya gesi kupitia kampeni ya PIKA KISASA NA SALAMA na wanawake 50 wajawazito wamepata vifaa vya kujifungulia kutoka Binti Salha Foundation, inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji – Salha Aziz (@salhabintiaziz) kwa Kushirikiana na wadau wa maendeleo Oryx Energies na Mdee Pharmacy.

Afisa Tarafa wa Pawaga, Emmanuel Ngabuji, amewahimiza wanawake kubadili mtazamo, kuwa tayari kubadilika na kutumia Nishati safi kwa usalama wao na mazingira huku Diwani wa Ilolo Mpya Bw. Fundi Mihayo, akitoa shukrani kwa taasisi hiyo kwa mchango wake muhimu.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *