#HABARI: Watu nane wa familia moja ambao ni wakazi wa Kitongoji cha Omukigando cha Kijiji cha Kashambya kilichopo Kata ya Gera, wilayani Misenyi, mkoani Kagera wamenusurika kifo baada ya nyumba wanayoishi inayomilikiwa na Edwin Kaishozi, anayefanya shughuli zake nchini Uganda, kuchomwa moto na watu ambao hawajafahamika waliokuwa na madumu ya petrol na silaha mbalimbali vikiwemo visu ambavyo kwa pamoja walivitelekeza kwenye eneo la nyumba hiyo.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania