#HABARI: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyeregete iliyopo Kata ya Rujewa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya, ambao baadhi yao hulazimika kutembea umbali wa kilomita kumi na mbili kufuata elimu, wameiomba Serikali kuwajengea mabweni ili waweze kutumia muda mwingi kwenye masomo na kuwaepusha na vishawishi mitaani.
Baada ya wanafunzi kueleza kilio chao,mkuu wa mkoa wa Mbeya Dkt Juma Homera akaeleza mkakati wa Serikali na kuiagiza halmashauri ya Mbarali kupitia bajeti ujayo watenge fedha kiasi cha shilingi milioni mia moja na ujenzi wa bweni uanze kwa haraka.
Serikali katika kuendelea kuboresha mazingira ya walimu wanaofundisha Vijijini imejenga nyumba mbili za kisasa za two in one kwa gharama ya shilingi milioni mia moja, wakati Mkuu wa mkoa akizindua ndipo wanafunzi wakaeleza kilio chao cha kutumia muda mwingi wakiwa barabarani kuelekea shuleni kutafta elimu.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania