#HABARI: Wanafunzi wa kike wa shule za msingi na Sekondari wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kupatiwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ili kuepuka ugonjwa huo .
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu Mkoa wa Manyara Dkt. Andrew Method wakati akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo kwa Walimu wa shule za Msingi na Sekondari Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara kuhusu Uhamasishaji wa chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV).
Aidha, mafunzo mengine yaliyotolewa ni pamoja na magonjwa mengine yanayozuilika kwa chanjo, lishe, afya ya uzazi kwa vijana balehe, lishe, usafi wa mazingira na umuhimu wa uanzishwaji wa Klabu za Afya shuleni.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania