#HABARI: Wakulima wa zao la Mahindi, wilayani Handeni, mkoani Tanga, wameomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwapatia dawa ya kuulia wadudu wanaoshambulia zao hilo kwa kasi.
Kamera ya ITV imetembelea baadhi ya mashamba yalioathirika na kuweza kuzungumza na baadhi ya wakulima huku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Bw. Mussa Mkombati, ameelezea changamoto hiyo na kuwaagiza wataalam wa kilimo kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania