#HABARI: Wakulima wa korosho mkoani Mtwara, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Us…

#HABARI: Wakulima wa korosho mkoani Mtwara, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Us…

#HABARI: Wakulima wa korosho mkoani Mtwara, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika (Korosho Cooperative Joint Enterprise – KCJE), kwa hatua ya kuhakikisha pembejeo za korosho zinawafikia kwa wakati unaofaa msimu huu wa kilimo.

Wakulima hao wamesema kwa mara ya kwanza tofauti na misimu iliyopita pembejeo zimefika mapema kabla ya kuanza kwa shughuli za kilimo jambo ambalo limeleta faraja kubwa kwao na kuwawezesha kujiandaa kikamilifu, kwani imekuwa mwarobaini wa changamoto sugu za upatikanaji wa pembejeo na vifungashio kama magunia ya kuhifadhia korosho, ambayo hapo awali yalikuwa adimu au ghali kupatikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *