#HABARI: Shirika la Taifa la Nyumba (NHC), mkoani Kilimanjaro, limeziondoa kwa nguvu familia saba zilizokuwa zinaishi kwenye nyumba mbili za shirika hilo mjini Moshi, bila kulipa kodi baada ya mmiliki halali ambaye ni baba wa familia hizo kufariki dunia na kuachia watoto wake nyumba hizo kinyume cha sheria.
Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Juma Kiaramba, amesema baada ya mmiliki halali kufariki nyumba hizo zilitakiwa kirejeshwa kwenye shirika hilo.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania