#HABARI: Shirika la Masoko ya Kariakoo linatarajia kuendesha mnada wa nafasi kwa wafanyabiashara wanaotaka sehemu za kufanya bia…

#HABARI: Shirika la Masoko ya Kariakoo linatarajia kuendesha mnada wa nafasi kwa wafanyabiashara wanaotaka sehemu za kufanya bia…

#HABARI: Shirika la Masoko ya Kariakoo linatarajia kuendesha mnada wa nafasi kwa wafanyabiashara wanaotaka sehemu za kufanya biashara soko jipya la Kariakoo kwani soko hilo limeshakamilika kwa asilimia 98 ambapo mnada huo utafanyika kupitia mfumo wa TAUS.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA Ashiraph Yusuph Abdulkarim Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari namna wanavyoendelea kuratibu wafanyabiashara waliokuwepo kurejea kwenye soko hilo ambapo kwa idadi walikuwa 1520 lakini hadi sasa waliojisajili kwenye mfumo na kujaza fomu ni wafanyabiashara 1159 na kusema kuwa maeneo mengine ya wazi yaliyobaki yatatangazwa Juni 2 kupitia mfumo wa TAUSI ili yapate wapangaji.

“Natoa wito kwa wananchi wote taasisi za umma na binafsi kuchangamkia fursa ya kupata maeneo ya kufanya biashara katika soko jipya la Kariakoo kwani bado kuna maeneo ya wazi yanahitaji kujazwa baada ya kuwa tumewarejesha wale wa awali waliokuwepo,” ametoa rai CPA Abdulkarim.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *