#HABARI: Serikali ya Marekani inaripotiwa kufikiria kuweka vikwazo vya usafiri au marufuku kabisa ya kuingia kwa raia wa nchi 36, zikiwemo 25 kutoka bara la Afrika.
Washington inataka nchi hizo zitimize baadhi ya masharti ya usalama na zimepewa siku 60 za kutimiza masharti hayo.
Nchi 36 zitakabiliwa na marufuku hiyo, zikiwemo nchi 25 za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Côte d’Ivoire, Gambia, Niger, na Senegal, kulingana na memo ya ndani ambayo Gazeti la Washington Post limepata kopi na baadaye na shirika la habari la Reuters.
Hati hiyo iliyotiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, ilitumwa siku ya Jumamosi, Juni 14, 2025, kwa wanadiplomasia kutoka nchi husika. Nchi hizo zina siku 60 kutimiza baadhi ya masharti.