#HABARI: Serikali imetangaza kulifutia usajili Kanisa la Ufufuo na Uzima, linalomilikiwa na Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwaj…

#HABARI: Serikali imetangaza kulifutia usajili Kanisa la Ufufuo na Uzima, linalomilikiwa na Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwaj…

#HABARI: Serikali imetangaza kulifutia usajili Kanisa la Ufufuo na Uzima, linalomilikiwa na Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima, ikiwa ni siku moja tangu kiongozi huyo wa kiroho atangaze msimamo wake wa kuendelea kukemea vitendo vya utekaji na watu kupotea.

Kufutwa kwa kanisa hilo kumetangazwa kupitia barua iliyoandikwa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel R. M. Kihampa.

“Katika siku za hivi karibuni, kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, umeonekana ukiwa katika mimbari ya Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church@ Kanisa la Ufufuo na Uzima, ukitoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya
kuichonganisha Serikali na wananchi.

“Vitendo hivi ni kinyume cha Sheria ya Jumuiya Sura ya 337 chini ya kifungu cha 17 kikisomwa pamoja na kifungu cha 39 cha Sheria
Namba 3 ya Mwaka 2019 kwa kuwa vinaathari ya kuhatarisha amani na utulivu nchini.

“Hivyo, kwa Mamlaka niliyopewa chini ya Kifungu cha 17(b) cha Sheria ya Jumuiya Sura ya 337 kikisomwa pamoja na kifungu cha 39 cha Sheria Namba 3 ya mwaka 2019 kilichoifanyia marekebisho kifungu cha 2 cha Sheria ya Jumuiya, nikujulisha kuwa
nimefuta usajili wa Glory of Christ Tanzania Church @ Kanisa la Ufufuo na Uzima, kuanzia leo tarehe 02 Juni 2025. Unatakiwa kusitisha shughuli za Kanisa lako mara moja.”

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *