#HABARI: Serikali imesema huduma za afya ya akili zimeshajumuishwa kwenye vifurushi vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), n…

#HABARI: Serikali imesema huduma za afya ya akili zimeshajumuishwa kwenye vifurushi vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na hivyo wananchi wanaonufaika na bima wanaweza kupata matibabu hayo kwa mujibu wa mwongozo wa matibabu uliopo.

Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Jesca Msambatavangu, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa, huduma za afya ya akili, ushauri nasaha, pamoja na huduma za kibingwa kama vile utengamao, zote zimetajwa kama huduma muhimu kwenye Mwongozo wa Matibabu (Standard Treatment Guideline – STG) na zinagharamiwa na NHIF.

Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa huduma za afya ya akili zinapewa uzito sawa na huduma nyingine za msingi, na kuimarisha upatikanaji wake kupitia mifumo ya bima ya afya kwa wote.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *