#HABARI: Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi, ametuma salamu za pole kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mk…

#HABARI: Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi, ametuma salamu za pole kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Mhe. Cleopa David Msuya, kilichotokea leo katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt.Mwinyi amesema atamkumbuka Mzee Msuya kwa mchango wake katika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa Serikali alizotumikia enzi za uhai wake.

Aidha Rais Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, familia ya marehemu, ndugu na marafiki na Watanzania kwa ujumla.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *