#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameona mchoro wa Barabara ya Mzunguko wa Nje ya Jiji la D…

#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameona mchoro wa Barabara ya Mzunguko wa Nje ya Jiji la D…

#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameona mchoro wa Barabara ya Mzunguko wa Nje ya Jiji la Dodoma (Dodoma Outer Ring Road) katika eneo la Mtumba, mkoani Dodoma, na hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo mkubwa, unaolenga kupunguza msongamano jijini Dodoma na kuimarisha usafirishaji wa watu na bidhaa.

Rais Samia ameshuhudia mchoro huo akiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk Akinwumi Adesina, wakati akifanya ziara ya kukagua ujenzi barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma, ambapo Rais Samia amekagua maendeleo ya ujenzi huo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo, akiendeleza ajenda ya maendeleo ya kitaifa kupitia miradi mikubwa ya kimkakati.

#Follow @radioonetanzania

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *