#HABARI: Rais Samia Suluhu Hassan, amependekeza barabara ya mzunguko ya Dodoma ipewe jina la Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrik…

#HABARI: Rais Samia Suluhu Hassan, amependekeza barabara ya mzunguko ya Dodoma ipewe jina la Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrik…

#HABARI: Rais Samia Suluhu Hassan, amependekeza barabara ya mzunguko ya Dodoma ipewe jina la Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk Akinwumi Adesina, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya miundombinu nchini.

“Katika kumuwekea Kumbukumbu na kwa kutambua mchango wake na mchango wa Benki ya maendeleo ya Afrika katika kuimarisha sekta ya usafiri na usafirishaji Tanzania, nimeridhia pendekezo la Waziri wa Ujenzi la kuwa barabara hii ya mzunguko ya nje ya Jiji la Dodoma iitwe kwa jina lake, Nitumie fursa hii kutangaza rasmi kuwa barabara hii ya mzunguko nje ya Jiji la Dodoma itaitwa barabara ya Dkt. Akinwumi Adesina.” Amesema Rais Samia.

Dkt. Samia amebainisha hayo wakati wa hotuba yake kwa wananchi wa Dodoma mara baada ya kukagua ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa Msalato na barabara hiyo ya mzunguko, akimtakia mema Dkt. Adesina katika mipango yake ya baada ya kustaafu.

“Tanzania imeweza kuvutia mitaji kutoka kwa wabia muhimu kama benki ya AFDB kutokana na kuwepo kwa utulivu na amani, sera nzuri za kiuchumi, usimamizi thabiti wa miradi ya maendeleo na kujituma kwa watanzania wenyewe kujenga nchi yao.

#Follow @radioonetanzania

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *