#HABARI: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe

#HABARI: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe

#HABARI: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amesema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imejidhatiti kuhakikisha inadhibiti vitendo vya rushwa kabla, wakati na hata baada ya Uchaguzi Mkuu huku akiwaasa wagombea kujiepusha na vitendo vya rushwa huko majimboni kwani TAKUKURU ipo kazini.

Mhe.Sangu amebainisha aya Wilayani Nzega Mkoani Tabora na kueleza kuwa kitendo cha Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa jumla ya magari mapya 195 kwa ajili ya TAKUKURU ni uthibitisho tosha kuwa anachukia vitendo vya rushwa

Amesema TAKUKURU itawakamata wale wote watakaothubutu kutoa rushwa ya aina yeyote ile kwa lengo la kuwarubuni wapiga kura “Msikubali kurubuniwa na rushwa na atakayethubutu kufanya hivyo toeni taarifa kwa TAKUKURU”Amesisitiza Mhe. Sangu.

Amesema mbali ya kutoa magari hayo, katika kipindi chake cha uongozi Rais. Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, ametoa fedha za kujenga jumla Ofisi 25 katika mikoa na Wilaya mbalimbali nchini kwa lengo la kuwawezesha watumishi wa TAKUKURU kufanya kazi katika mazingira rafiki hususan katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu

#Follow @radioonetanzania

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *