#HABARI: Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Afya, Profesa Tumaini Nagu, amesema serikali imeendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa zaidi ya asilimia 85, katika vituo vyote vya afya nchini huku akisisitiza wananchi kuhakikisha wanakuwa na bima ya afya, ili kupunguza gharama za matibabu jambo ambalo litasaidia huduma hizo kuwa endelevu.
Ameyasema hayo Chalinze mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kufuatilia hali ya utoaji wa huduma za afya pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Kwa upande wake Mmkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bwana Ramadhani Possi amesema Halmashauri hiyo imetenga milioni 300 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania