#HABARI: Mzee Flavian Methew Nyandikuu mweye umri wa miaka 85 mkazi wa Kunduchi Mtongani Kilongowima jijini Dar es Salaam amelia na ofisi ya Kamishina wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushindwa kumlikisha ardhi yake kwa zaidi ya miaka 40 sasa ambapo kila akienda katika ofisi hizo kudai haki yake amekuwa akizungushwa na kupewa majibu yasiyokuwa na tija na hivyo sasa amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro huo ili haki yake ipatikane.
Wakizungumza kwa niaba ya mzee huyo ambaye kwa sasa anazungunza kwa shida kutokana na uzee wake, mtoto Happy Flavian amesema kutokana mgogoro huo afya ya baba yake imezidi kutetereka.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania