#HABARI: Mwanamke aliyetoweka baada ya mumewe kuuawa kikatili walipokuwa kwenye fungate yao amekamatwa baada ya kujisalimisha, polisi wa India wamesema.
Familia za wanandoa hao zilidai kuwa bibi harusi pia alikuwa ameuawa au kutekwa nyara, na wakaanzisha msako mkubwa kumtafuta.
Miongoni mwa waliokamatwa ni mkewe bwana harusi Sonam Raghuvanshi mwenye umri wa miaka 25, kuhusiana na mauaji ya Raja mwenye umri wa miaka 30.
Babake Sonam, Devi Singh, alimtetea binti yake, akisema, “Yeye hana hatia, hawezi kufanya hivi.”
Wapenzi hao wapya, wanaoishi Indore, Madhya Pradesh, walichagua Meghalaya kwa fungate yao kwa sababu walisikia kuwa ina “mabonde mazuri sana”, kakake Raja, Sachin Raghuvanshi alisema kabla ya Sonam kukamatwa.
Wenzi hao walifunga ndoa mnamo Mei 11 huko Indore katika sherehe ya harusi yenye baraka za familia zao zote mbili.
“Ndoa yao ilipangwa miezi minne kabla ya siku yenyewe. Wote wawili walikuwa na furaha sana, hakukuwa na mzozo wowote kati ya wawili hao kabla au baada ya ndoa,” alisema kaka mwingine wa Raja, Vipin Raghuvanshi.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania