#HABARI: Mtoto mchanga mwenye jinsi ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki mbili, amekutwa ametelekezwa njiani eneo la Kituo cha Mabasi Bweri mkoani Mara na mama yake mzazi ambaye hakuweza kufahamika, kisha kuacha ujumbe wa maandishi uliosomeka “ameshindwa kumlea mtoto huyo kwa sababu ya ugumu wa maisha na yeye ni mwanafunzi.”
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amethibitisha kuokotwa kwa mtoto huyo na kudai kwa sasa huyo amehifadhiwa katika kituo cha kulelea watoto cha Bweri Senta.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania