#HABARI: Moshi mweusi umetoka kwenye bomba la paa la Kanisa la Sistine, Vatican, ukiashiria kwamba Papa mpya bado hajapatikana

#HABARI: Moshi mweusi umetoka kwenye bomba la paa la Kanisa la Sistine, Vatican, ukiashiria kwamba Papa mpya bado hajapatikana.

Makardinali 133 wataendelea kupiga kura siku ya Alhamisi kwa siri hadi watakapompata mrithi wa Papa Francis, hakuna jina lililopata theluthi mbili ya kura zinazohitajika kumpata kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki.

Maelfu ya waumini waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, walishuhudia tukio hilo kwa utulivu, huku wakisubiri kwa matumaini ishara ya moshi mweupe – ishara ya kupatikana kwa Papa mpya – ambayo haikutokea.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *