#HABARI: Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw.Adam Malima amesisitiza wafugaji kuhakikisha Ng’ombe wote wanaofugwa wasigeuke sababu ya mi…

#HABARI: Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw.Adam Malima amesisitiza wafugaji kuhakikisha Ng’ombe wote wanaofugwa wasigeuke sababu ya mi…

#HABARI: Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw.Adam Malima amesisitiza wafugaji kuhakikisha Ng’ombe wote wanaofugwa wasigeuke sababu ya migogoro badala yake mifugo hiyo ifugwe kwa tija na kuzalisha maziwa bora kwa ajili ya kuboresha afya za Watanzania na kutengeneza ajira.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Wakili Sebastian Waryuba, amesema hayo wakati akizindua wiki ya maziwa kitaifa ikiwa na kauli mbiu “Maziwa salama kwa afya bora na uchumi Endelevu”.

Kwa upande wake Msajili wa bodi ya maziwa nchini Prof.George Msalya akabainisha licha ya virutubisho vingi vinavyopatikana kwenye maziwa pia yana mchango mkubwa kuzalisha ajira huku Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Sospeter Mtwale akisema watatumia maadhimisho hayo kuelimisha Watanzania.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *