#HABARI: Mgombea Urais wa Upinznai nchini Colombia Miguel Uribe Turbay yupo kwenye hali mbaya baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa anaongea na Wananchi katika eneo la Bogota, Polisi nchini humo wamethibitisha.
Video mtandaoni inaonesha Miguel akihutubia kisha baadaye akapigwa risasi zilizomfanya kumwaga damu nyingi ambapo amepelekwa Hospitali anakoendelea kutibiwa.