#HABARI: Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imetekeleza jukumu la kuandaa rajamu (Nation Brand Mark),ili kupat…

#HABARI: Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imetekeleza jukumu la kuandaa rajamu (Nation Brand Mark),ili kupat…

#HABARI: Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imetekeleza jukumu la kuandaa rajamu (Nation Brand Mark),ili kupata alama itakayotambulisha bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini (Made in Tanzania) katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Sehemu ya awali ya mchakato wa kupokea bunifu za alama ya Taifa ya bidhaa na huduma za Tanzania, umekamilika ambapo alama takribani 88 kutoka kwa Watu mbalimbali ziliwasilishwa na zikipatikana 6.

Watu sita waliobuni alama hizo walipata mafunzo kwa ajili ya awamu ya pili ya shindano ambapo kutoka mwa Wabunifu hao 6, alama 3 bora zimepatikana na sasa zimewekwa hadharani kwa Umma ili zipigiwe kura kwa njia ya mtandao na alama itakayoshinda ndio itakayosajiliwa kwa ajili ya matumizi.

Kati ya alama hizi tatu unadhani ipi inastahili kuibika Mshindi?, tafadhali pigia kura chaguo lako na Mshindi atatangazwa siku ya uzinduzi rasmi wa alama ya Taifa ya bushaa na Huduma za Tanzania, ambapo siku ya uzinduzi itatangazwa baadaye.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *