#HABARI: Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, imebaini mbinu mpya ya kuwatumia wazee kifanikisha biashara hiyo hiyo haramu, baada ya watendaji wa mamlaka hiyo kumkamata zee David Solomon Akiyoo, Mwenye miaka 76 akisafirisha zaidi ya gunia kumi za bangi.
Akizungumza kwà niaba ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas James Lyimo wakati wa kuteketeza bangi hiyo ,mmoja wa Maafisa wa Mamlaka hiyo Bw.Benson Mwaikenda amesema mzee huyo amekamatwa katika operesheni zinazoendelea.
Mwaikenda ameitaka jamii kuachana na biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya kwani zinawaongezea umasikini usio wa lazima suala ambalo pia limezungumziwa na baadhi ya wananchi.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania