#HABARI: Mama mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa Wanging’ombe aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la uvimbe kwenye kizazi na kupeleke…

#HABARI: Mama mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa Wanging’ombe aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la uvimbe kwenye kizazi na kupeleke…

#HABARI: Mama mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa Wanging’ombe aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la uvimbe kwenye kizazi na kupelekea changamoto ya kutoshika ujauzito ambapo alibahatika kushika ujauzito na mimba kutoka mara tatu mfululizo, amefanyiwa upasuaji na Madaktari Bingwa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa na Daktari Bingwa wa Uzazi na Kizazi Dkt. Chuma Novacatus mara baada ya kufanikisha upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye kizazi uliofanyika katika Hospitali ya Halmashauri ya Wanging’ombe mkoani Njombe.

Dkt. Novacatus ameeleza kuwa uvimbe huo umesababisha kusukuma kuta za ndani za kizazi na kutokwa na damu kwa muda mrefu, ambako pia kulimsababishia kupata changamoto ya kutoshika ujauzito, hata alipobahatika kushika ujauzito mimba zilikuwa zinatoka zinapofikia miezi mitatu au minne.

“Mama huyo amekuwa akihudhuria katika vituo vya afya mbalimbali na kupatiwa huduma lakini bado hakupata nafuu,” ameeleza Dkt. Novacatus.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *