#HABARI: Makadinali wenye dhamana ya kupiga na kupigiwa kura wanakutana katika baraza la siri kuchagua Papa mpya

#HABARI: Makadinali wenye dhamana ya kupiga na kupigiwa kura wanakutana katika baraza la siri kuchagua Papa mpya.

Mkutano huo wa siri unafanyika katika kanisa dogo la Sistina, Mei 7 ukijumuisha makadinali 135 kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Mkutano huu unafuatia kifo cha Papa Francis, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 88 siku ya Jumatatu ya Pasaka Aprili 21, na mazishi yake kufanyika siku ya Jumamosi Aprili 26.

Hakuna muda maalum uliowekwa kumchagua Papa mpya, lakini mikutano miwili ya awali ya uchaguzi wa Papa iliyofanyika mwaka 2005 na 2013, ilidumu kwa siku mbili tu.

Kwa zaidi ya miaka 750, sheria kali zimetawala orodha ya makadinali wanaokusanyika kumchagua papa. Na kumekuwa na usiri mkubwa wa kuzuia taarifa kutoka nje kuingia ndani na za ndani kutoka nje.

Makadinali wakisalia na utumishi zaidi kwenye kuchagua kuliko ushawishi wowote. Kwenye kulinda usiri hata baadhi ya vyakula vinazuiwa kuingizwa ndani.

Kwa mfano kuku ni kitu ambacho kimepigwa marufuku kutoka kwenye meza ya makadinali kwa karne nyingi, kwani vinaweza kutumika kupitisha ujumbe wa siri.

Kuna makadinali 252 kote ulimwenguni kufikia tarehe 19 Februari 2025, ambao kwa kawaida pia ni maaskofu. Na wale walio chini ya umri wa miaka 80 ndio wanaostahili kumpigia kura papa mpya.

Idadi ya “makadinali wanaopiga kura” kwa kawaida hupunguzwa hadi 120, lakini kwa sasa kuna makadinali 135 kati yao ambao wana vigezo vya kushiriki katika kumchagua Papa mpya. (Papa Francis aliteua Makadinali wapya 21 mwezi Desemba 2024.)

Hii ndiyo idadi kubwa zaidi ya makadinali wenye umri wa kupiga kura katika historia ya Kanisa Katoliki.

Makadinali ni washiriki wakuu wa makasisi wa Kanisa Katoliki na kwa kawaida huwekwa wakfu kuwa maaskofu.

Papa Francis aliteua idadi kubwa ya makadinali wenye umri wa kupiga kura, 108, wakati wengine walichaguliwa na watangulizi wake Papa Benedict XVI na Mtakatifu John Paul II.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *