#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Lushoto, imemhukumu mwalimu wa Madrasa Abuubakar Hamis, mkazi wa eneo la Dule B lililopo Jimbo la Bumbuli wilayani humo, baada ya kukutwa na hatia ya Kumlawiti mara kwa mara Mtoto wa kaka yake wa kiume, ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la pili na kumsababishia athari kubwa kiafya.
Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu wa Wilaya Mh. Rose Ngoka, kabla ya hukumu kutolewa mwanasheria wa Serikali na Mwendesha Mashtaka wa shauri hilo wilayani Lushoto Sylivia Mitanto, amesema mtuhumiwa alikuwa akimlawiti mara kwa mara mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akikaa kwa bibi yake, baada ya wazazi wao kutengana.
Pia amesema Bibi wa mwanafunzi huyo alikuwa akifahamu kitendo hicho, anachofanya mwanaye kwa mtoto wa kaka yake, ndipo alipojitokeza msamaria mwema na kutoa taarifa kwa wanasheria.
Akifafanua zaidi bada ya taarifa hizo kufika katika Vyombo vya sheria mtuhumiwa alimuadhibu vibaya mwanafunzi huyo, kwa kuvujisha siri hadi shauri hilo lilipotolewa maamuzi, na kusababisha mwalimu huyo wa Madrasa kwenda Jela maisha katika Ngome Kuu ya Gereza la Maweni.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania