#HABARI: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeahirisha kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha De…

#HABARI: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeahirisha kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha De…

#HABARI: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeahirisha kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu hadi Julai 1, 2025.

Uamuzi huo umetolewa ili kumpa muda Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuendelea kupitia jalada la kesi hiyo na kufanya maamuzi ya iwapo shauri hilo litapelekwa Mahakama Kuu au la.

Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Franko Kiswaga, baada ya ombi la upande wa mashtaka likiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga.

Katuga aliiambia Mahakama kuwa jalada la kesi hiyo bado lipo kwa DPP anayelipitia na kutoa maelekezo kuhusu hatua za upelelezi na iwapo shauri hilo linapaswa kuhamishiwa Mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Lissu anadaiwa kutenda kosa la uhaini Aprili 3, 2025, katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo anadaiwa kwa nia ya uchochezi, kuushawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, pamoja na kutoa matamshi yenye lengo la kumshinikiza kiongozi mkuu wa Serikali ya Tanzania.

Tarehe 2 Juni 2025, upande wa Mashtaka ulieleza Mahakama kuwa jalada la upelelezi liliwasilishwa kwa DPP, lakini baada ya kulipitia alibaini kuwepo kwa mapungufu yaliyohitaji kurekebishwa na hivyo kuliwasilisha tena kwa wapelelezi.

Kutokana na hali hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga aliomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine, ambapo Hakimu Kiswaga alikubali na kupanga kesi hiyo kutajwa tena Julai 1, 2025.

#Follow @radioonetanzania

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *