#HABARI: Kuelekea Uchaguzi Mkuu Mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Stephen Wasira amewaagiza Viongozi…

#HABARI: Kuelekea Uchaguzi Mkuu Mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Stephen Wasira amewaagiza Viongozi na Wajumbe wa Chama hicho kusikiliza kero za Wananchi kwenye vikao vyao na kuzitatua haraka kwa sababu Wananchi ndio wenye Maamuzi ya Nchi katika kuleta Mendeleo Nchini.

Agizo hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Stephen Wasira kwa njia ya Simu kwenye kikao cha wajumbe wa Chama cha Mapinduzi wa Matawi yote ya Jiji la Mbeya chenye lengo la kueleza Miradi iliyotekelezwa na Serikali pamoja na kutatua Kero za Wananchi amabcho kimeongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Mkoa wa Mbeya Ndele Mwanselela.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Mkoa wa Mbeya Ndele Mwanselela amewataka Wanachama wote wa Chama hicho kuendelea kuungana kwa pamoja bila kujali Chama chochote na kusemea Mapmbo mazuri yaliyofanywa na Chama.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *