#HABARI: Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Jun…

#HABARI: Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Jun…

#HABARI: Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Juni 16, 2025.

Kesi hiyo imeahirishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franko Kiswaga mara baada ya kusikiliza hoja za upande wa Jamhuri na upande wa utetezi.

Awali, Upande wa Jamhuri uliomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa kuwa upelezi haujakamili hoja ambayo ilipingwa vikali na upande wa utetezi wakidai upelelezi umechukua muda mrefu.

Akitoa majumuisho, Hakimu Franko Kiswaga, aliuuliza upande wa Jamhuri kwamba upelelezi umefikia wapi ambapo ulijibu hatua za mwisho hivyo kutaka upelezi huo ukamilishwe haraka kwa kwa kuwa upo katika hatua ya mwisho na kesi iweze kuendelea.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *