#HABARI: Katika kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth), Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Dkt. Damas Ndumbaro, ameeleza kuwa mpango wa msaada wa kisheria unaoendeshwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umevuka mipaka ya taifa na sasa unatajwa kuwa mfano wa kuigwa duniani kote – hasa kwa nchi wanachama wa madola.
Mpango huo, ambao umelenga kuwafikia wananchi wa kawaida – hasa wanawake, watoto, na makundi yaliyo katika mazingira magumu – umepewa sifa kwa jinsi unavyoboresha upatikanaji wa haki kwa watu wasio na uwezo wa kumudu gharama za huduma za kisheria.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania