#HABARI: Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, CPA. Amos Mkalla, amepiga goti kuwaomba wakazi Mvomero, wamruhusu aendelee kumsaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. Samia Suluhu Hassan na kwamba sasa siyo wakati muafaka kwa yeye kugombea Ubunge kwa kuwa, ana kazi kubwa aliyepewa na Mwenyekiti wake katika kazi za chama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
CPA. Makalla ambaye alikuwa Mbunge wa zamani wa Mvomero, amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika Mtibwa Morogoro, kwenye ziara yake ya Mkoa wa Morogoro, licha ya mbunge wa sasa wa Mvomero, Bw. Jonas Van Zeeland, kuahidi kuwa endepo CPA. Makalla atachukua fomu yeye hatochukua na badala yake atamuunga mkono.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania