#HABARI: Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Mhe

#HABARI: Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Mhe. Maryam Ahmed Muhaji ametoa wito kwa jamii kuunganisha nguvu za pamoja katika kusaidia wasichana shuleni ili kupata taulo za kike katika kustawisha hedhi salama na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.

Bi. Mariam amesema hayo wilayani Babati Mkoani Manyara wakati wa mafunzo kwa baadhi ya wanafunzi na walimu pamoja na wadau wengine wa Afya mkoani Manyara na ngazi ya taifa umuhimu wa matumizi sahihi ya taulo za kike na utambulisho wa mradi wa usambazaji wa taulo za kike kutoka Kampuni ya Real Relief kupitia mradi wa SAFEPAD na kampuni ya A to Z.

Afisa Programu kutoka Mpango wa Taifa wa Afya na Lishe Shuleni , Wizara ya Afya Dkt. Julietha Tibyesiga amesema hedhi salama inapozingatiwa ni namna bora ya kumtunza msichana shuleni ili aweze kusoma vizuri huku akizungumzia Maandalizi ya Mwongozo wa Usimamizi wa Hedhi salama.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *