#HABARI: Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa usalama wa nishati ni nguzo muhimu katika uwepo wa usalama wa nchi, maendeleo endelevu, ustawi wa jamii na uhifadhi wa mazingira hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika miradi mikubwa ya kuzalisha nishati safi na ya uhakika.
Mhandisi Mramba amesema hayo wakati wa Mkutano wa Kitaifa wa Usalama wa Taifa (National Security Symposium 2025) uliofanyika jijini Arusha ambao umekutanisha wataalam wa sekta ya Nishati na Usalama.
“Nishati si jambo la anasa, ni hitaji la msingi kwa maisha ya kila Mtanzania na ni injini ya maendeleo ya taifa lolote, hivyo usalama wa nishati unapaswa kuangaliwa kama ajenda ya kimkakati ya ulinzi wa Taifa,” amesema Mhandisi Mramba
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania