#HABARI: Kampuni ya Apple imetoa ushauri kwa baadhi watu wenye tabia ya kuweka simu kwenye mchele kama njia ya kukausha maji yal…

#HABARI: Kampuni ya Apple imetoa ushauri kwa baadhi watu wenye tabia ya kuweka simu kwenye mchele kama njia ya kukausha maji yal…

#HABARI: Kampuni ya Apple imetoa ushauri kwa baadhi watu wenye tabia ya kuweka simu kwenye mchele kama njia ya kukausha maji yalioingia kwenye simu kuacha kabisa tabia hiyo kwani inaweza kuharibu simu.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, punje ndogo za mchele zinaweza kuingia kwenye sehemu ya kuchaji, zikachubua sehemu za ndani na hata kunasa unyevu unaoweza kuharibu simu kwa kutu.

Kampuni hiyo ya Apple imependekeza njia mbadala ya kutatua changamoto hiyo ya simu kuingia maji kwa kuzima simu mara moja na tenganisha na nyaya au vifaa vyote, na kutikisa kwa upole huku ukiwa umeshikilia sehemu ya chaji ikiwa chini ili kutoa majimaji.

Iache ikauke kwa hewa katika sehemu yenye ubaridi na hewa ya kutosha, na kisha hakikisha imekauka vizuri kabla ya kujaribu kuichaji tena.

#Follow RadioOneStereo

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *