#HABARI: Kamishina wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amezindua kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ya umeme inayokwenda na kaulimbiu ya PIKA SMART.
Mha. Luoga amezindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Shirika la Modern Energy Cooking Services (MECS) chini ya ufadhili wa UKAID kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Nishati.
Mhandisi Luoga amesema kampeni hiyo imezinduliwa ikiwa ni mojawapo ya jitihada za Serikali kuhakikisha inawahamasisha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia ili kufikia lengo la asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.
#Follow @radioonetanzania
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.