#HABARI: Kamati ya Bunge ya Wizara ya Fedha imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa…

#HABARI: Kamati ya Bunge ya Wizara ya Fedha imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa…

#HABARI: Kamati ya Bunge ya Wizara ya Fedha imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa hatua muhimu ya kuhuisha viwango vya mafao kwa wastaafu pamoja na uanzishwaji wa mfumo mpya wa kujihakiki unaotarajiwa kuanza kutumika kuanzia Julai 1, 2025.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Mheshimiwa Twaha Mpembenwe, wakati akisoma maoni ya Kamati kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na makadirio ya bajeti ya mwaka 2025/2026 Bungeni mjini Dodoma

Mheshimiwa Mpembenwe amesema kuwa mfumo huo mpya wa kujihakiki utapunguza kero kwa wastaafu waliokuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu ili kufuatilia mafao yao, hivyo kuwawezesha kupata huduma kwa urahisi zaidi na kwa wakati.

Aidha, Kamati imeeleza kuwa hadi kufikia mwezi Aprili 2025, kiasi cha shilingi trilioni 1.78 kilikuwa tayari kimepokelewa, sawa na asilimia 82.2 ya bajeti, hali inayoashiria utekelezaji mzuri wa mipango ya kifedha ya Serikali.

#itvdigital #itvupdates #itvtanzania.

#follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *