#HABARI: Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha Huduma ya Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi.Ester Msambazi, amewataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo jirani, kuchangamkia fursa ya huduma za Msaada wa Kisheria zinazotolewa bure na Serikali kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid, kwenye banda la Wizara ya Katiba na Sheria lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya NaneNane Nzuguni Jijini humo.
Bi. Ester amesisitiza kuwa huduma za msaada wa kisheria bure kwa Wananchi zitatolewa viwanjani hapo hadi tarehe 8 Agosti 2024.
“Wananchi watumie siku hizi kwa ajili ya kuja kupata huduma za msaada wa kisheria lakini kwa wale walio nje ya Mkoa wa Dodoma wanaweza kufika kwenye mashirika yanayotoa huduma za Msaada wa Kisheria katika maeneo yao, ili kuweza kupata huduma hizo kule kule walipo’’Amesema Bi. Ester.
(Feed generated with FetchRSS)