#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia kikosi cha Usalama barabarani kimefanya ukaguzi maalumu wa mabasi ya abiria kwa …

#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia kikosi cha Usalama barabarani kimefanya ukaguzi maalumu wa mabasi ya abiria kwa …

#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia kikosi cha Usalama barabarani kimefanya ukaguzi maalumu wa mabasi ya abiria kwa ajili ya kudhibiti ajali kutokana na uwepo wa ongezeko kubwa la abiria kufuatia kuanza kufungwa kwa Shule.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed, ameleza hayo wakati akizungumza na madereva katika Stendi kuu ya mabasi Mkoani humo na kwamba msimu huu wanafunzi wengi wanasafiri kuelekea mikoani hivyo kunasababisha kuwepo kwa ongezeko la abiria.

SSP Zauda amebainisha kuwa kutokana na ongezeko hilo la abiria pamoja na magari binafsi, madereva wanapaswa kuendesha magari yao kwa tahadhari kubwa huku wakizingatia na kufuata sheria za usalama barabarani wakati wote ili kuepuka ajali.

Pia amewataka madereva hao pindi wanapopata changamoto barabarani ikiwepo kuharibika kwa magari yao kuhakikisha wanayaondoa na kuyaweka pembeni au kuweka alama ambazo zitasadia watumiaji wengine wa barabara kuona.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *