#HABARI: Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja ametangaza kupatikana kwa bunduki iliyotumika kumpiga risasi na kumuua Mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo, katika barabara ya Ngong jijini Nairobi wikiiliyopita.
Bunduki hiyo ni kati ya bastola mbili zilizopatikana kutoka kwa watuhumiwa wawili waliokamatwa usiku wa Jumanne katika Mtaa wa Chokaa Kayole jijini Nairobi.
Watuhumiwa hao wawili Edwin Oduor Odhiambo, anayejulikana kwa jina jingine kama Abdul Rashid na Dennis Sewe Manyasi wanaongeza idadi ya waliokamatwa kuhusu mauaji hayo hadi nane. Dereva na mlinzi wa Mbunge huyo ambao walikuwa na mbunge huyo wakati wa mauaji yake wanazuiliwa baada ya kutoa taarifa zinazokinzana baada ya mauaji hayo. Maswali yakiibuka kuhusu ni jinsi gani mlinzi wa mbunge huyo aliyekuwa amejihami hakuwezi kufyatua risasi yoyote wakati mbunge huyo alipopigwa risasi tano zilizomuua.