#HABARI: Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) nchini Kenya, imewasimamisha kazi Maafisa watano walioko katika Kituo Kikuu cha Polis…

#HABARI: Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) nchini Kenya, imewasimamisha kazi Maafisa watano walioko katika Kituo Kikuu cha Polis…

#HABARI: Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) nchini Kenya, imewasimamisha kazi Maafisa watano walioko katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Nairobi, kuhusiana na kifo cha Albert Omondi Ojwang, ambaye alifariki dunia akiwa kizuizini.

Katika taarifa ya waandishi wa habari iliyotolewa Jumatatu, Juni 9, NPS ilithibitisha kusimamishwa kwa Afisa Mkuu wa Kituo cha Polisi, OCS, afisa aliyekuwa kazini usiku huo, afisa anayesimamia Seli, na maafisa wote ambao walikuwa kazini usiku huo.

Inspekta Mkuu wa Polisi, Douglas Kanja, aliagiza kuchukuliwa kwa hatua hiyo kuruhusu uchunguzi ufanyike kwa ukamilifu, usio na upendeleo, na wa haraka juu ya suala hilo ambao unaongozwa na chombo huru cha kusimamia polisi nchini Kenya (IPOA).

“Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) bado imejitolea kuhakikisha utekelezaji wa sheria, haki za binadamu, uwazi, na uwajibikaji ndani ya huduma hii,” alisema taarifa ya NPS.

Babake Ojwang, Meshack Opiyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa mwanaye alikamatwa kutokana na chapisho kwenye mtandao wa X katika mji wa magharibi wa Homa Bay na kisha kusafirishwa kilomita 350 hadi mji mkuu, Nairobi.

Awali, taarifa ya polisi ilieleza kuwa, “Akiwa kizuizini, mshukiwa alipata majeraha kichwani baada ya kujigonga kwenye ukuta wa seli,” Alikimbizwa hospitalini “ambapo alitangazwa kuwa amefariki dunia”.

Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International tawi la Kenya aliiambia BBC kwamba kifo cha Bw Ojwang, aliyeelezwa kama mwalimu na mwanablogu, kinatia shaka sana.

Amnesty ilisema katika taarifa yake kwamba kifo chake kinaibua maswali mazito ambayo lazima yachunguzwe kwa haraka, kwa kina na kwa uhuru.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *