#HABARI: Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU LTD, kimefanikiwa kusafirisha korosho zilizobanguliwa zenye thamani ya shilingi milioni 208 kwenda nchini Uingereza, ikiwa ni hatua nyingine kubwa katika kukuza soko la nje kwa mazao ya wakulima wa mkoa wa Mtwara.
Hayo amebainishwa na Meneja Mkuu wa TANECU LTD, Bw. Mohamed Mwinguku, na kueleza kuwa jumla ya Tani 14.8 za korosho zilizobanguliwa zimesafirishwa zikiwa na thamani ya Dola za Kimarekani 77,400, sawa na shilingi milioni 208 za Kitanzania.
Amesema mafanikio haya ni matokeo ya jitihada za makusudi zinazofanywa na chama hicho, katika kuhakikisha korosho za wakulima zinapata thamani zaidi kupitia ubanguaji na usafirishaji wa moja kwa moja kwenda kwa wanunuzi wa kimataifa.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania