#HABARI: Askari Polisi James Mukhwana amefikishwa mahakamani Milimani na Halmashauri Huru ya Kuangazia Utendakazi wa Polisi (IPO…

#HABARI: Askari Polisi James Mukhwana amefikishwa mahakamani Milimani na Halmashauri Huru ya Kuangazia Utendakazi wa Polisi (IPO…

#HABARI: Askari Polisi James Mukhwana amefikishwa mahakamani Milimani na Halmashauri Huru ya Kuangazia Utendakazi wa Polisi (IPOA) kwa kuhusika moja kwa moja na mauaji ya mahabusu Albert Ojwang katika selo za polisi za Kituo cha Polisi cha Central jijini Nairobi.

IPOA wameomba muda wa siku 21 kumshikilia afisa huyo wa polisi aliyekuwa na funguo za selo za polisi wakati wa kifo cha mwalimu Albert kwenye selo za polisi wakati wanapokamilisha uchunguzi katika kesi ya kifo cha Ojwang. Afisa huyo kupitia wakili wake Danstan Omari amepinga ombi la IPOA.

Awali, kijana wa miaka 23 aliyekiri kuharibu kamera za CCTV katika Kituo cha Polisi cha Central, Kelvin Musymi Mutava amekiri kulipwa shilingi 3000 kuharibu ushahidi siku aliyouawa mahabusu Ojwang.

#Follow @radioonetanzania
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *