Mwanasiasa huyo John Heche amesema chama hicho kitaendelea kuheshimu maamuzi ya mahakama kuu iliyopiga marufuku viongozi wa chama kutojihusisha na siasa wala utumiaji mali ya chama.
Amesema kutokana na mazingira hayo, chama hicho sasa kinawaelekeza wafuasi na wanachama wake kuendelea kujishughuli na masuala ya kisiasa bila kuathiri maamuzi ya mahakama na wakati huo huo kujishughuli zaidi na mambo ya kijaamii ikiwamo upandaji miti, kushiriki shughuli za ibada na mikusanyiko mingine ya kawaida.
“Amri ya zuio la kutojishughulisha na shughuli za siasa imeelekezwa kwa katibu mkuu na bodi ya wadhamini”, alisema.
Heche amesema ajenda ya chama hicho bila mabadiliko hakuna uchaguzi mkuu inaendelea kusalia pale pale na amewahimiza wanachama wake kuendelea fulana zinazobeba ujumbe huo.
Ama awali, Jeshi la polisi nchini Tanzania lilizua mkutano uliokuwa umeitishwa na chama Chadema na waandishi wa habari uliokuwa umepangwa kufanyika katika hoteli moja jijini Dar es salaam.
Jeshi hilo kandaa maalumu wa Dar es salaam limesema mkutano huo ulikuwa siyo halali na hivyo kuwaamuru waandishi wa habari pamoja na baadhi ya viongozi wa chadema kutawanyika katika eneo la tukio.
Heche ndiye aliyepanga kuzungumza na waandishi wa habari lakini azma hiyo haikutumia baada ya maofisa wa polisi kupiga marufuku mkutano huo.
Polisi yazuia mkutano wa Heche
Heche ndiye aliyepanga kuzungumza na waandishi wa habari lakini azma hiyo haikutumia baada ya maofisa wa polisi kupiga marufuku mkutano huo.
Mapema waandishi wa habari walikuwa wameanza kumimini katika eneo la ukumbi wa hoteli ya Seashells, kujiandaa na mkutano na mwanaisasa huyo uliopangwa kufanyika kuanza nyakati za saa sita mchana.
Hata hivyo, muda chahe kabla ya muda huo kuwaadia maafisa wa polisi walifika katika eneo la hoteli hiyo na kisha kwenda moja kwa moja katika chumba na 511 ghorofa ya tano na kutoa amri ya kuwataka waandishi hao kufungasha vifaa vyao na kuondoka mara moja.
Baadaye maofisa hao wa polisi walitoa amri ya kuwataka kuondoka baadhi ya wale walionekana kuwa wafuasi na viongozi wa chadema walikuwa wamefika katika eneo hilo la hotel ambao baadhi yao walikuwa wamevalia fulana zenye ujumbe usemao ” bila mabadiliko hakuna uchaguzi”.
Magari mawili ya polisi yaliendelea kusalia katika eneo la hoteli hiyo yakipiga doria kwa saa kadhaa kabla ya baadaye kuondoka.
Hivi karibu mahaka kuu ya Tanzania ilitoa amria ya kuwapiga marufuku viongozi wa chama hicho kutojihusisha na shughuli za kisiasa pamoja na kutogusa mali za chama hicho hadi pale kesi iliyoko mahakami itakamomalizika.
CCM na ACT wajiandaa kwenda kwenye uchaguzi
Hatua hiyo inakuja wakati vugu vugu la kuelekea katika uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu likiwa linaanza kupanda kwa baadhi ya vyama vya siasa. Akitoa tathmini yake kuhusu yale yanayoendelea kwa chadema na hatma ya uchaguzi mkuu, mchambuzi wa mambo Gwandumi Mwakatobe anasena uchaguzi wa mwaka huu huenda ukakosa hamasa kutokana na mazingira yanayoendelea kuibuka.
Tayari chama tawala CCM na baadhi ya vyama vya upinzani ikiwamo ACT Wazalendo ni baadhi ya vyama ambavyo vimekuwa vikipanga kuelekea katika uchaguzi huo wa rais, wabunge na madiwani uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba.