#HABARI: Serikali kupitia Wizara ya Afya imejenga jumla ya wodi 165 za kuhudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) katika hospitali mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha huduma za afya kwa watoto wachanga.
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, ametoa taarifa hiyo Bungeni jijini Dodoma leo Juni 17, 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Asha Abdullah Juma, aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kushughulikia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.
Dkt. Mollel amesema idadi hiyo imeongezeka kutoka wodi 14 zilizokuwepo awali hadi kufikia 165 mwaka 2024, huku Serikali ikilenga kufikia hospitali 280 zenye huduma hizo ifikapo Desemba 2025.
#Follow RadioOneStereo
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.