#HABARI:Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura amefanya uhamisho wa Makamanda watatu, ambao ni Kamishna Msaidizi Mwandam…

#HABARI:Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura amefanya uhamisho wa Makamanda watatu, ambao ni Kamishna Msaidizi Mwandam…

#HABARI:Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura amefanya uhamisho wa Makamanda watatu, ambao ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Dodoma.

Nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Galus Hyera, ambaye amehamishwa kutoka Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli, kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Aidha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Matride Kuyeto, amehamishwa kutoka Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayofanyika ndani ya Jeshi la Polisi, katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

#Follow @radioonetanzania

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *