#HABARI: Shirika lisilo la kiserikali la Miico, linalojihusisha na masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo usalama wa chakula, lis…

#HABARI: Shirika lisilo la kiserikali la Miico, linalojihusisha na masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo usalama wa chakula, lis…

#HABARI: Shirika lisilo la kiserikali la Miico, linalojihusisha na masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo usalama wa chakula, lishe bora na kilimo himilivu, kupitia mradi wake wa Nourish kwa kushirikiana na Shirika la T Mark, limeanza kutoa elimu ya lishe bora pamoja na mbinu za malezi kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ili kukomesha hali ya udumavu inayotajwa kuongezeka wilayani Momba, mkoani Songwe.

Akiwa katika Kijiji cha Ikana, Kata ya Ikana, wilayani humo ambapo limefanyika zoezi la utoaji elimu, namna ya kupika chakula bora kwa kuzingatia makundi yote ya vyakula, Afisa Miradi wa shirika hilo Bi. Frimina Kavishe, amesema pamoja na uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi katika eneo hilo bado linakabiliwa na hali ya udumavu hivyo wametoa elimu ya kilimo cha mazao mengine ya mboga mboga ikiwemo maharage na alzeti.

Kwa upande wake Bi. Veronica Komanya, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba, kando na kupongeza mkakati huo wa shirika la Miico, amewataka wananchi wa eneo hilo kuifanyia kazi elimu walipewa yenye lengo la kuondoa udumavu katika jamii hiyo kupitia mradi huo unaotekelezwa kwa miaka mitano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *