#HABARI: Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wametoa azimio la kumuunga mkono…

#HABARI: Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wametoa azimio la kumuunga mkono…

#HABARI: Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wametoa azimio la kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa utendaji mzuri wa kazi anazofanya katika sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, elimu pamoja na kumkomboa mwanamke kiuchumi.

Akisoma azimio hilo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bi. Rehema Sanga, amesema mambo mbalimbali ambayo yaliyopelekea kuandaa azimio hilo ikiwemo uboreshaji wa huduma za afya kwa mama na mtoto zilizopelekea kupunguza vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Edward Mpogolo, akipokea azimio hilo amelipongeza jukwaa hilo kwa kuandaa maazimio hayo kwani wametambua kazi njema ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezifanya na kuwaomba wanawake wengine kuendelea kumuunga mkono Rais Samia, kwani kufanya hivyo ni kumtia moyo na kutambua thamani yake.

#Follow @radioonetanzania

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *