#HABAI: Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina, amepongeza jitihada na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu na ya Kimkakati, akiahidi kuwa Benki hiyo itaendelea kuwa Mbia wa Serikali ya Tanzania, katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Rais Dkt. Adesina amebainisha hayo leo wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Samia Mkoani Dodoma leo muda mfupi mara baada ya Rais Samia kukagua utekelezaji wa ujenzi wa uwanja wa Kimataifa wa ndege Msalato pamoja na ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa Kilomita 112.3.
Katika salamu zake, Dkt. Adesina amemtaja Rais Samia kama Kiongozi wa mfano barani Afrika na duniani kote kutokana na namna ambavyo ameendelea kufanikisha maendeleo kwenye sekta mbalimbali nchini sambamba na jitihada zake katika kuimarisha utengamano wa Kikanda.
#Follow @radioonetanzania
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.